Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?
Na Godfrey Nangeda.
Vuguvugu la katiba mpya, ndio habari inayo chukua nafasi,
katika vyombo mbali mbali vya habari, na mijadala yake imefika maeneo tofauti
tofauti ya watu. Makazini, vijiweni, mitaani, na sehemu mbali mbali katika
jamii. Watoto wa mjini wanasema,’ katiba mpya ndo habari ya mjini’.
Jambo moja la kutafakari na la kujiuliza katika hili ni? Nani mkweli kati
ya Tume ya Jaji Joseph SindeWarioba, Ukawa naTanzania kwanza?
Mamlaka zilizopo kihalali kwa mujibu wa sheria.
Tume ya Jaji Warioba
Mchakato wa kupata katiba ya Jamhuri ya Muungano ulianza
kwa kutungwa
Sheria
ya Mabadiliko ya Katiba na baadaye kupitia sheria hiyo Tume ya
kukusanya
maoni ya wananchi ikaundwa kwa ajili ya kukusanya maoni na
kuandaa
rasimu ya katiba. Kwa mujibu wa sheria hiyo ya mabadiliko ya katiba
kwa
sasa tumebakiza hatua mbili ili kukamilisha mchakato wa katiba. Hatua
hizo ni Bunge la Katiba na kura za maoni . Hatua zote za
mchakato wa kupata katiba zinatofautiana na zina mamlaka
tofouti na
zinapaswa
kuwa shirikishi kwa wananchi wote.
Katika
taifa lolote lile msingi wa uendeshaji wa Taifa hutegemea sana sheria
kuu
. Katiba huainisha tunu na misingi ya nchi yoyote, pia hutoa
migawanyo
na ukomo wa madaraka na majukumu mbalimbali ya mihimili mikuu
ya
dola. Kutokana na umuhimu huu mchakato wa katiba ni lazima uwe
shirikishi
katika ngazi zote .
Katiba
ina paswa kuzingatia mambo ya wananchi ili kuifanya waimiliki na kuiheshimu
katiba hiyo kwani wao ndio wenye mamlaka na taifa lao na namna gani wangependa
liwe.
Ukiwa
na Katiba ambayo wananchi hawakushiriki vizuri, lazima Katiba hiyo
itakuwa
vigumu kupata utekelezaji na umiliki wa wananchi.
Historia
inatusuta kuwa mipango na michakato mingi ya kikatiba baada ya kupata uhuru
haikuwashirikishi bali ilihusisha tu viongozi. Katiba
ya kwanza ya Tanganyika ya
1961
ilipatikana kupitia Bunge la Kikoloni, katiba ya 1962 ilipatikana kupitia
white
paper na sheria ya Bunge la Katiba ikatumika kugeuza bunge la kawaida
kuwa
Bunge la Katiba, hali kadhalika katiba ya Muungano ya 1964 na ile ya
Muda
ya 1965 zote hazikupata Baraka za wananchi. Mwaka 1977 Katiba yetu
inayotumika
hadi leo iliundwa na kamati ya chama iliyogeuzwa kuwa tume ya
katiba
na baadae tume hiyo kupeleka maoni yake na mitazamo kwa Kamati Kuu ya Chama
cha
Mapinduzi (CCM). Kamati hii ya Chama ndiyo ilipeleka rasimu kwenye
Bunge
ili kujadiliwa na kupitishwa. Michakato yote hiyo haikushirikisha wananchi
tofouti
na huu wa sasa, wa tume ya jaji Warioba na wajumbe wake.
Kwa
namna moja au nyingine tume imefanya ilicho fanya na kutuletea ilicho kuta kama
ilivyo tumwa,(kukusanya na kuratibu,siokutengeneza katiba), baada ya tume
kutuletea ilicho pata kutoka kwa wananchi, yakaanza maneno ya chini chini,
baadae yakawa ‘maneno ya juujuu. ’
Wapo
waliooipongeza kazi yatume, wapo pia walioilani tume, kwangu mimi wote hawa
hawaninjimi usingizi, kwa sababu tunaishi katika dunia ambayo tunatofautiana
mambo mengi, kuanzia malezi, ushirika katika maswala mbali mbali ya kijamii,
elimu tulizo nazo tuna tofautiana maslahi, kwahiyo lazima tuwena mitazamo
tofauti kwani tuko tofauti, ilatofauti zetu inabidi zituletepamoja katikakupata
katiba bora.
Tanzania kwanza,
hiki ni kikundi cha watu wanaosema wanatetea katiba ya
wananchi,ukiwaangalia watu hawa kwa
undani kidogo, utakuta ni wale wajumbe wote, ambao mtazamo wao una randana au
unafanana, na wajumbe wanaotoka CCM, na wale wote wakundi la miambili na moja
wanao shabihiana na msimamo wa chama tawala, hawa wanajiita wanatetea maoni ya
wananchi, na wanaamini mfumo uliopendekezwa na tume ya Mzee Warioba una
mushkeli kwa Taifa kwa siku za usoni. Pia ukiwasikiliza vizuri wanajenga hoja
kwamba mbona kuna maooni ya mabaraza ya katiba baadhi yao yaliachwa na tume,
halafu wanakwenda mbali wana sema kuna baadhi ya mikoa mbona maooni yao ni
kiduchu sana.
Kwao
wanaona pia kuna asilimia kubwa ya watu
hawakupendekeza mfumo huu unaopigiwa chapuo na tume ya Jaji warioba.
Kwahiyo
wanaona mchakato huu haukua halali sana na wala sio mzuri.
Naomba
maswali yanguyaanzie hapa, unaweza kushaanga kwanini sikuanza maswali na tume, sababu
ya msingi ni kwamba tume hiihaijawahi kupewa nafasi na mamlaka zilizopo ili
iieleze utata unaojitokeza kulingana na
makundi mbali mbali ya wanajamii wanavyo chambua hizo rasimu zake, ilizo
wasilisha, narudia tena tume hii haijawahi kupewa nafasi ya kuelezea utata
wowote unaoonekananamakundi mbali bali yawana jamii, kikubwa kilicho fanywa na
mamlaka ni kujaribu kuifuta(delete)sio kifuto cha kawaida na kufunga tovuti
yake, kumbuka maneno yamzee Butiku kwamba “kuna vitabu vya tume vilifichwa day
one” badala yake zimejitokeza taassisi na asasi mbali mbali na vyombo vya
habari vya binafsi vinavyo jaribu kuwaelewesha watu nini tume ilimaanisha,
wakati mwingine muktadha na maantiki ya mijadala hiyo inakuwa migumu kuifanyia uchambuzi jadidi
kwa kuwa hatujui misimamo, mitazamo na sera za vyombo hivyo au hizo taasisi, kwa hi hiyo
tunashindwa kutoa hukumu sahihi, isiyo kuwa na mawaa.
Tanzania kwanza,
kundi hili halipo kisheria na wala hatujui wamejipanga vipi kimkakati na lengo
lao mwisho wa safari ni nini, limeibuka tu kama uyoga au kama alivyo ibuka Babu
wa Samunge Loliondo, Hatuoni mipango madhubuti,wala dhima nzima iliyoko nyuma
yao bali tunacho kiona kwa kua walioko kwenye uongozi, (wenyewe wanajisikia
raha ukiwaita walio kwenye utawala), kwa kua wana taka hicho basi na wafuasi
wote wanao shabikia kundi hili wote wanafuata hivyo hivyo, mwisho wa safari
sijui watajikuta wapi, mimi na wewe yetu macho.
Kundi
hili limejinasibu linashabikia serikali mbili, au uundwaji wa katiba ya
wananchi itakayo tambua nchi moja yenye serikali mbili,(ingawa sasa hatuna nchi
moja angalia mabadiliko ya katiba ya Zanzibar 2010) wanasema wanachi hawataki
tatu kwani tatu ni mzigo, sijui lini walikwenda kwa wananchiwakapata maooni
hayo ya serikali mbili, kwani wote tunakubaliana tume ya warioba ilikuwa
kisheria kwenda kufanyakazi iliyo tumwa,ndio maana wote hawa hawasemi tume
haikuwa kisheria kufanya kazi iliyo ifanya,wote wanaitambua tume na kazi iliyo
fanya, kwa hiyo wote wanakubaliana tume imefanyakazi na kazi hiyo ina tambuliwa
tofauti yao ni kwamba, hiki tume ilicholeta wengine wanakubali ni sahihi, na
wengine wanakataa wanasema kina walakini.
Kwenu
njie mnao kataa kazi ya tume kwamba si sahihi, lini mliitaka tume iwaeleze
kinaga ubaga wa hizo taarifa zake , lini mliitaka tume iwafafanulie icho msicho
kielewa?
Watu
wamebaki kupayuka na kutengeneza propaganda, mara tume haikutumwa hivyo, mara
mzee warioba kafanya yakwake nasio yawananchi. Swali la msingi nyie mnao
simamia serikali mbili lini mlikwenda kukusanya maoni kwa wananchi mkaja na
hiyo rasimu ya wananchi ina yo akisi maoni ya hizo serikali mbili?, binafsi huwanasema utafiti hujibiwa kwa
utafiti, na sio blabla.
Kundi
hili limejipambanua hadharani namna lilivyo na linacho kitaka. Tatizo
lakundi hili halina sehemu ya kujificha kama tutakavyo ona wenzao wa ukawa.
Ndio maana linaonekana ni baya na halifai katika mstakbali wa kupata katiba
bora.
Ukichunguza
kwa undani kidogo utakuta wala sio wananchiwanao watetea bali wanajaribu
kuhakikisha mambo yana kwenda watakavyo ili maslahi yao yalindwe.
Kwani
wana amini endapo mfumo ukibadilika hata maslahi yao yata kuwa shakani, kwa
hiyo fanya ufanyavyo bora punda afe mzigo wa mfalme ufike.
Ukawa, wanajiita umoja wa katiba yawananchi, mchezo ni uleule
kama wa wenzao Tanzania kwanza,
maslahi mapana ya wanasiasa, hakuna jipya hapa, kama walivyowenzao wanafanya
propaganda za kudai wana tetea msimamo wa wananchi wa tume ya Warioba wenye
mapendekezo ya serikali tatu.
Uzuri kidogo wa hawa mabwana, wanasehemu ya
kujificha, wanajificha kwenye mwanvuli wa tume yam zee Warioba, na kwakua
wananchi wengi wanapenda kusikia mambo ya tume ya jaji Warioba kwahiyo wana bebwa
mzobemzobe lakini wenyewe wanaamini endapo tume ya Warioba maoni yao
yakiheshimiwa basi uchaguzi mwakani 2015 utakuwa laini kwao, na CCM itaangushwa
na wao kuchukua nchi(poor thinking).
Katiba
si swala la kisiasa pekee wala si swala la kisheria pekee, bali pia katiba
niswala lamaridhiano, namna tutakavyokubaliana
na kwapamoja kuelewana ni namna gani tungependa sote kwa pamoja nchi yetu
iweje, ijiendesheje, ni swala la sisi sote
tunapangaje mambo yetu na tungetegemea tuendesheje.
Hata
ikifikia tukakubaliana kusiko kukubaliana, basi iwe yote hayoni kwa maslahi ya
sisi sote na vizazi vijavyo vya taifa hili.
Napenda
kurudia tena si kikundi cha Tanzania kwanza wala Ukawa wanao dai kwamba wana
akisi maoni ya wananchi, wote hawa wamejikita katika mrengo wa kisiasa wakufikiri
mfumo fulaniukikubaliwa utakuwa nafuu kwao na wala sio maslahi mapana ya taifa
hili.
Tume
ya kukusanya maoni angalau ina weza kujinasibu imefanya kazi iliyotumwa na
ukweli tume hii hakuna hata mtu mmoja
anaeikataa tume hii au aliyependekeza tofauti wakati inaapishwa na wakati ina
kwenda kufanya kazi iliyo tumwa. Kizungumkuti kinatokea baada ya tume kuleta
kitu ambacho baadhiya wakubwa wetu wanaona kama ni dhihaka kwao.
Vikundi
hivivyote viwili kwa asilimia kubwa vinatokana na wabunge wavyama tofauti
tofauti, wakajaribu kujikusanya na
kutengeneza umoja wao, hawa wakajiita Ukawa, wengine Tanzania kwanza ingawa
ndani yao kunawafuasi wanao penda misimamoyao.
Mwisho
kwa kuhitimisha makala yangu ni ngependa kuwataka watanzania wote tuache
maslahi mepesi ya baadhi ya viongozi mbalimbali ambao tunawapenda, na tuache
ubinafsi wakutanguliza matumbo yetu, kwa
kutetea au kujificha nyuma ya mfumo fulani tukiamini utakuwa jibu mujarab
kwa maslahi yetu, tupende kujaribu kufuatilia
mambo kwa kina na tuweke mstakbali mpna wa kutengeneza katiba bora kwa manufaa
ya taifa zima.
Tujitaidi kuangalia viongozi tunao waamini
wana malengo na taifa hili,? Au ni maslahi tu,tupime kaulizao na matendo yao
kama hazina maono mema tuwakimbie, kwani taifa hili ni letu sote na sisi sote
ni ndugu.
Sisi sote ni ndugu.
0717008781/0756314274
No comments:
Post a Comment