MICHEZO

Etoile kutua Tanzania usiku wa manane

  • Dakika 17 zilizopita
Etoil du Sahel
Wapinzani wa Yanga timu ya Etoile du Sahel kutoka Tunisia wanatarajiwa kuwasili saa 9 usiku kuamkia Ijumaa kwa usafiri wa Ndege ya kukodi ya kampuni ya Nouvelair bj 4870 wakiwa na msafara wa watu 56.
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tunisia (FTF), Krifa Jalel ndiye mkuu wa msafara huo akiwa na Rais wa klabu ya Etoile du Sahel (ESS) Charefeddine Ridha, wachezaji 19, benchi la ufundi lenye watu 13, waandishi wa habari 12 na wanachama 10
Timu ya Etoile du Sahel itafikia katika hoteli ya Ledger Plaza zamani Bahari Beach eneo la Kunduchi, na Ijumaa wanatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Waamuzi wa mchezo huo ni Samwel Chirindiza, Arsenio Marenguka, Celio de Jesus Musabe, Jose Maria Bachide wote kutoka nchini
Msumbuji na walitarajiwa kuwasili mchana wa Alhamisi, huku kamisaa wa mchezo huo Salah Ahmed Mohamed kutokea
nchini Sudan akitarajiwa kuwasili leo jioni na wote watafikia katika hoteli ya Protea iliyopo Oysterbay.






Sepp Blatter akwezwa

  • Saa 9 zilizopita
Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter anayekubalika na wengi.
Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter amefananishwa na manabii waliopita, kama vile rais wa zamani wa Afrika kusini hayati Nelson Mandela pamoja na Winston Churchill wakati wanachama kumi wa shirikisho la soka la Amerika ya kaskazini, America ya kati na muungano wa visiwa vya Caribbea (Concacaf) wakimuunga mkono kiongozi huyo katika uchaguzi wa FIFA hapo May.
Azimio hilo la kumuunga mkono Blatter limefanywa katika mkutano wa (Concacaf). Rais wa chama cha soka cha jamhuri ya Dominic Osiris Guzman, amemfananisha rais huyo wa FIFA na watu mashuhuri walioweka historia duniani ikiwemo Moses, Abraham Lincoln na Martin Luther King.
“Jumuia inatuma ujumbe kuw tunaendelea kumuunga mkono Blatter” alisema rais wa Concafaf Jeffrey Webb.Blatter ambaye ni raia wa Uswiss ni mmoja kati ya wagombea wa nne. Wengine ni pamoja na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Ureno Luis Figo, Mholanzi Michael van Praag, na mwana mfalme Prince Ali Bin Al Hussein ambaye alikuwa pamoja na Blatter katika mkutano huo wa Alhamis japokuwa akuhutubia.







Wenger:Walcott kusalia Arsenal

  • 16 Aprili 2015
Walcott na mkufunzi Arsene Wenger
Meneja wa kilabu ya Arsenal Arsene Wenger ana imani kwamba Theo Walcot ataweka mkataba mpya na kilabu hiyo ya Ligi ya Uingereza.
Walcot mwenye umri wa miaka 26 amesalia na mwaka mmoja katika kandarasi yake na anahusishwa na uhamisho wa kujiunga na kilabu ya Liverpool.
Alipoulizwa kuhusu kusalia kwa Walcot katika uwanja wa Emirates,Wenger alisema kuwa nina imani kuwa Walcot ana maisha mazuri mbeleni.
Mshambuliaji huyo ameanza mechi tano pekee msimu huu huku akiendelea kuuguza jeraha la mguu alilopata msimu uliopita.
Lakini mchezaji huyo wa Uingereza ambaye amefunga mabao 77 katika mechi 203 alizochezea Arsenal huenda akajumuishwa katika kikosi cha mechi ya semi fainali ya kombe la FA dhidi ya Reading.
''Amerudi kutoka katika jeraha baya sana na kila wiki anaimarika'',Wenger alisema.








 brazili yugu
STARS YALALA 4-2 DHIDI YA BOTSWANA

No comments:

Post a Comment