Thursday, July 31, 2014

UMUHIMU WA KUTUNZA MAZINGIRA KWA FAIDA YANGU NA YAKO.

UMUHIMU WA KUTUNZA MAZINGIRA KWA FAIDA YANGU NA YAKO.

Na Godfrey Nangeda.













Wapendwa leo tutaangalia kidogo upande tofauti, naule tuliozoea, leo tuko upande wa mazingira, kwani endapo tutayaboresha basi na shughuli zetu za kiujasiriamali zitaweza kufanyika vizuri sana, karibu sasa twende pamoja.

Monday, July 28, 2014

MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA KWA MJASIRIAMALI

Mjasiriamali ni mtu anayepaswa kila wakati kuwa na macho yanayo ona mbali, katika shughuli zake za biashara aifanyayo au huduma aitoayo. Leo nimeandaa mambo kadha kwa mjasiriamali yoyote atakae zingatia ita kuwa ni faida kwake, na shughuli aifanyayo.

Nimeandika kwa kifupi sana lakini ukweli yanaeleweka na ukiyatilia maanani ni msaada mzuri kwako.
Mambo yenyewe ni kama yafuatayo.

MAMBO YA KUZINGATIA KWA MJASIRIAMALI KILA SIKUKATIKA  SHUGHULI ZAKE.

1.JITAIDI KUWAMTUWAKWANZA KUJUA KINACHOTOKEAKATIKA ULIMWENGU WA BIASHARA NA FURSA MPYA ZA KUWEKEZA.

2.KUWAMVUMILIVUKATIKA SHUGHULI YAKO NA JITAIDI KUFANYAMABADILIKO CHANYAILIBIASHARA YAKO IWEMPYA KILA UCHAO.

3.PENDA KUZINGATIA UBORA NA UFANISI KATIKA HUDUMA YAKO, ACHA KUKIMBILIA PESA ZA KIPINDI KIFUPI, JENGA MSINGI IMARAWAKUPATA FEDHAWAKATI WOTE.

4.USISITE KUTHUBUTU KUANZISHA SHUGHULI YOYOTE,AU BIASHARAYOYOTE, CHA KUZINGATIA FANYA UPEMBUZI WA SOKO, ALAFU  JIKITE KATIKA BIASHARA UITAKAYO.

5.JITAIDI KUPANGA MAMBO KISASA, KAMA  H UNAUJUZI SANA ENEOHILI USISITE KUWAONA WATAAALAMU WA BIASHARA..

6.TENGENEZA MTANDAO NA WATUMBALIMBALI,WATAKAO KUWA MSAADA KATIKA SHUGHULI YAKO,JENGA PIAUSHAWISHI KWA WATEJA NA WAFANYA BIASHARA WALIO FANIKIWA ZAIDI YAKO.

7.JIAMINI  KATIKA HUDUMA YAKO, NA HASA KAMA ULIIPANGA SAWASAWA,
Hapa ningependa kueleza kidogo, baadhi ya wafanya biashara wakitanzania haswawafanyabiashara wadogo, mtu akiwa chalenji kidogo kwenye biashara zao, majibu yao huwa mawili, kwanza ukimkuta mwenye mali anajiamini kidogo atamjibu mteja 'kama utaki weacha wenzio watanunua, sisi kila siku ndo tunavyo uza we nenda bwana unatutilia usiku tu, kama huna hela si useme usaidiwe,kukera biashara za wenzako tu'.  Ukimkuta mfanya biasha muoga, basi anashindwa hatakumjibu mtejawake, anakasirika kimya kimya, nakesho biashara hiyo anaacha kabisa, kisa "nimekwazwa".

Kama ikikutoke wewe usipandwe  na gadhabu jibu ni rahisi tu, kama ni kweli kuna kitu ulikosea mwambie "bwana pamoja na iyo shida kidogo uliyo iyona lakini bidhaa yetu ni bora una jaribu kumwonyesha kwamifano, namna bidhaa yenu ilivyo bora, au pia unamtaka radhi na kumwaidi mara nyingine utajitaidi kuboresha vizuri". Usikasirike ndugu, ingawa ni kweliwateja wengineujui aliko toka, jitaidi kuwa makini.

Kwa leo ni hayo tu ndugu zangu tutaonana wakati na mara nyingine.


Sisi sote ni ndugu,

Godfrey Nangeda
0717008781/0756314274

Friday, July 25, 2014

KWANINI NI VEMA KUWA MJASIRIAMALI?

Ujasiriamali ni mchakato wa kuziona fursa na kuweka miundombinu sahihi, pamoja na rasirimali watu,na rasirimali fedha kiasi katika eneo mahususi ili kufanya biashara au kutoa huduma, kwa lengo la kujiongezea kipato.
 Ujasiriamali una weza kuwa ni kufanya biashara, au kutoa huduma fulani, katika jamii.

Je ni kwanini kila mtu awe mjasiriamali?
Swali hili lina taka majibu yakina ili kuweka maana sawa ya umuhimu huo kwa jamii, na wanajamii wote.
Swali linginela kujiulizani kweli kila mtu ana sifa za kuwa mjasiriamali, labda ili uwe mjasiriamali unaitaji uwe na sifa zipi,(qualities)?

Ukweli wa mambo ni kwamba mambo mengine mengi una yo ambiwa kwamba unatakiwa kuwanayo ili uwe mjasiriamali pengine ni mengi sana na labda hauna wewe kama mtu binafsi na uka hisi basi wewe huna sifa za kuwa mjasiriamali.

Lakini kama utangulizi unavyo eleza ni hali au mchakato(process), wa wewe mtu binafsi, au kikundi mlioona fursa na kuzi changamkia, kwa lengo la kuwaongezea kipato, na kuwa fanya muishi kwa furaha.

Lengo kuu la kuwa mjasiriamali  ni moja tu au mawili kuongeza kipato, na kuweza kujijengea uwezo mzuri katika utendaji wa kazi zako za kila siku. Ujasiriamali ukifanywa kwa husahihi, una ibua mambo mengi na faida nyingi na kuku weka katika nafasi nzuri katika jammii yoyote, una weza kuaminiwa sana na kupata faida kubwa sana katika maisha.

Unaweza kupata mambo mengi lakini mimi na yaangalia mabo mawili kwa ujumla wake amboyo ndio chanzocha kuibua mambo mengine au faida nyingine.

Mambo hayo ni kuongeza kipata na kujenga utendaji mzuri katika shughuli zako.

Sasa swali la kujiuliza nani anafaa au ana sifa za kuwa mjasiriamali?

Inawezekana unajiuliza swali hili maranyingi sana na kujipima(assessment on qualities) kama na wewe una sifa za kuwa mjasiriamali.
Ukweli ni kwamba katika dunia hii tunayo ishi hakuna kinacho shindikana kama tu umetumia njia sahihi kupanga jambo lako, kisasa kisayansi haswa na lika shindwa kufanikiwa.



Kama litashindwa kufanikiwa basi kuna sababu pia za kisayansi zinazo pelekea jambo husika kutofanikiwa, yani na maanisha kuna( measurable reasons)sababu zinazo pimika kuonesha kukwama kwa jambo au kufanikiwa kwa jambo lolote. Kwahiyo swali  je! mimi nasifa za kuwa mjasiriamali? Jibu ni ndio wewe unazo hizo sifa, kikubwa ambacho una kosa ni fikra zako tu uja zi twist kwenye upande huo, wakuongeza mali katika kaya yako.

Kikubwa cha kufanya panga mambo yako kisayansi, panga mipango yako kwa weledi mkubwa,kuwa mvuumilivu katika kufanikiwa katika lengo kubwa zaidi. acha tamaa za muda mfupi jikite katika mambo ya maana, kuwa makini na matumizi ya fedha kwa mambo muhimu na yanayo itajika kwamaendeleo ya huduma uitoayo.

Kwahiyo ni swala la  wewe kutoka hapo katika mawazo uliyo nayo na kujaribu kuvuka mto wenye mamba wengi ukichukua njia sahihi na nakuhakikishia utafanikiwa.

Namna utakavyokuwa una endelea ndipo utaona wataalamu wengine, na watu wengine watakavyo kuwa wanakuja na kuanza kuonesha utaalamuwa na kukushauri  ili na lile, uta pata washa wazuri na wa baya kazi ni kwako kuchuja taarifa, ipi ina faida kwako na kwa wakati gani.

Shida kubwa ninayo iona watanzania tunayo ni kwamba, tuna weza kusoma vizuri au kusikiliza semina vizuri sana tukijaribu kuchukua hatua kidogo na endapo tuna kwama basi hapo ina kuwa ndo mwisho wa mchezo.

Nawatakia siku njema tutaonana wakati mwingine, chukua hatua usijione umechelewa, Mungu awabariki nyote.

Sisi sote ni ndugu.

Godfrey Nangeda.

Thursday, July 24, 2014

UMUHIMU WA KUWAJENGEA VIJANA UWEZO

Umasikini katika taifa letu umekuwa si jambo la kuwashangaza tena watu tunaowaamini,na ambao kwanamna moja ama njingine tuna aminini ndio injini ya kusaidia au kuchochea mabadiliko ya maendeleo katika jammii.
Mfanoo wa watuhao kama  Wasomi, wataalam wa maswala mbali mbbali,wanasheria, waalimu wadini, na watu wenye weledi wowote kwenye maswala mbalimbali ya nayo muhusu mwananchi. Kwanamna moja ama nyingingene, hawaoni au hawaguswi na matatizo moja kwa moja ya nao wakabili vijana katika kujikwamua na ugumu wa maisha unao wakabili.

Kuthibitisha haya niyasemayo, ni jinsi watu wote tulivyo kaa kimya tunapo shindwa kuwa na mikakati endelevu ya kuwajengea vijana uwezo hasa wanaotoka vyuoni, au ambao wako mtaani.
Tumekosa mbinu mujarabu yakuhakikisha hii rasirimali watu tunaitengenezea utaratibu mzuri ili ijikite kwenye uzalisha, nakusaidia nchi kupata maaendeleo ya haraka.

Binafsi sitaki kujikita katika muendelezo wa kulaumu mambo yalivyo au kuu laumu mfumo unao tuongoza kwanama tunavyo weza kuwasaidia au kujisaidia sisi sote kama taifa.

Hapa chini nimejaribu kuja  na angalau njia kadhaa ambazokwa namnamoja au njingine kama zita tumiwa au kufutwa na vijana zinawezakuwafanya ua kuwajengea vijana uwezo.,ili waweze kukabiliana nachangamoto za  maisha zinazo wakabili.


KWANZA VIJANA WAJITAIDI KUTAFUTA TAARIFA SAHII NA ZA WAKATI.
Taarifa sahii ndizo msingi  wakufanya mambo vizuri na kufikia mafanikio endelevu, ya mtu mmoja mmoja au taifa kwaujumla, swali  lamsingi  lakujiuli tarifa sahii tunazipata wapi?

Majibu ya swali hilo ni mepesi kabisa, taarifa sahii zinapatikana kwenye sekta husika, aushughulihussika, kwa mfano, unajiandakufungua kiwandakidogo cha usindikaji wa maziwa, nivizuri kupata maelekezo mazuri yana mna ya kuanzisha viwanda vidogo kwa watu kama SIDO wanao husika na viwanda vidogo vidogo. Taarifa ya SIDOitakuwa ni mwongozo mzuri kwamaendeleo ya kazi yako.

VJANA TUJIKITE KWENYE MAMBO YA MAANA.
Kwa namnamoja au njingine vijana tumepoteza muda mwingi kwenye mambo ambayo hayana tija kwetu wala kwa taifa, atupendi kudadisi mambo,tunaamini mambo yalivyo tubasi inatosha, tunapoteza rasilimali, muda, fedha na mabo kama hayo, mfano kijana ambaye hana kazi ya kueleweka anakuwa na uhusiano wa kimapenzi na kijanazaidi ya mmoja, hali hii wakati mwingine inatulazimu kutumia muda mwingi, na tunapoteza pesa nyingi na tunapata faida hasi kwenye matokeo hayo.

TUTENGENEZE MTANDAO WENYE MANUFAA.
Mtandao ni njia moja wapo inayo tuwezesha kuendesha mambo yetu kwa manufaa yetu, na taifaletu.
Mtandao una tuwezesha kupata hata taarifasahii  kwa ajili ya manufaa yetu. Niimaniyangu kwako kijana mwezangu kwamba kwa kupata taarifa sahii zitakuwa mwongozo sahihi  kwa mambo yako. Mfano unahudhuria semina,au maonesho ya sabasaba ni vizuri kuchukua mawasiliano yawatumbali mbalimbali kutegemea na taarifa unazo hitaji kulingana nashughuli yako, au uliyo panga kuifanya, mara nyingi tumetengeneza au tuna endelea kutengeneza mitandao yakututoa pesa zaidi badala ya kutengeneza mitandao ya kuingiza pesa zaidi  kwa maendeleo yetu.

TUJITAIDI KUPATA ELIMU NA TUPENDE KUSOMA TUKUZE FIKRA ZETU.
Shule ni mwalimu mzuri ili kufanikisha jambo kwa uhakika, tatizokubwa niliona lo kwa watanzania wote kuona elimu kama mzigo wa mawe, kwamba nikitu cha shida sana na kina uwekezaji mkubwa sana.
Hili lina wezakuwa ni jambo lakweli kutokana na mifumo yetuya kupata elimu na utoaji wake kwa jamii yetu. Elimu ilionekana, na bado inaoneka na kama anasa kuipata, na upatikanaji wake ni mgumu sana, inaonekana ni kwa watu wenye hela tu wanaowezakuipata, na ni kwatabusana.

Pamoja na yote hayo iyo isitumike kama sababu ya kimantiki kufifisha ari na hitaji la mtu mmoja mmoja kupata elimu. Lazma mamlaka husika na sisi wananchi mmoja mmoja tuwe na hamu ya kupata elimu na tuitafute kokote kwa udi na uvumba, kwani elimu bora ndio mstakbali wabaadae yetu.


Kwa leoni hayo machache ndugu kijana mwezangu, tujitaidi kubadilika kifikra,

Sisi sote ni ndugu.

Na Godfrey Nangeda.

Friday, July 11, 2014

BUNGE LA KATIBA

watanzania wanasubiri kwa hamu sana litakapo anza mwezi ujao