Mjasiriamali ni mtu anayepaswa kila wakati kuwa na macho yanayo ona mbali, katika shughuli zake za biashara aifanyayo au huduma aitoayo. Leo nimeandaa mambo kadha kwa mjasiriamali yoyote atakae zingatia ita kuwa ni faida kwake, na shughuli aifanyayo.
Nimeandika kwa kifupi sana lakini ukweli yanaeleweka na ukiyatilia maanani ni msaada mzuri kwako.
Mambo yenyewe ni kama yafuatayo.
MAMBO YA KUZINGATIA KWA MJASIRIAMALI KILA SIKUKATIKA SHUGHULI ZAKE.
1.JITAIDI KUWAMTUWAKWANZA KUJUA KINACHOTOKEAKATIKA ULIMWENGU WA BIASHARA NA FURSA MPYA ZA KUWEKEZA.
2.KUWAMVUMILIVUKATIKA SHUGHULI YAKO NA JITAIDI KUFANYAMABADILIKO CHANYAILIBIASHARA YAKO IWEMPYA KILA UCHAO.
3.PENDA KUZINGATIA UBORA NA UFANISI KATIKA HUDUMA YAKO, ACHA KUKIMBILIA PESA ZA KIPINDI KIFUPI, JENGA MSINGI IMARAWAKUPATA FEDHAWAKATI WOTE.
4.USISITE KUTHUBUTU KUANZISHA SHUGHULI YOYOTE,AU BIASHARAYOYOTE, CHA KUZINGATIA FANYA UPEMBUZI WA SOKO, ALAFU JIKITE KATIKA BIASHARA UITAKAYO.
5.JITAIDI KUPANGA MAMBO KISASA, KAMA H UNAUJUZI SANA ENEOHILI USISITE KUWAONA WATAAALAMU WA BIASHARA..
6.TENGENEZA MTANDAO NA WATUMBALIMBALI,WATAKAO KUWA MSAADA KATIKA SHUGHULI YAKO,JENGA PIAUSHAWISHI KWA WATEJA NA WAFANYA BIASHARA WALIO FANIKIWA ZAIDI YAKO.
7.JIAMINI KATIKA HUDUMA YAKO, NA HASA KAMA ULIIPANGA SAWASAWA,
Hapa ningependa kueleza kidogo, baadhi ya wafanya biashara wakitanzania haswawafanyabiashara wadogo, mtu akiwa chalenji kidogo kwenye biashara zao, majibu yao huwa mawili, kwanza ukimkuta mwenye mali anajiamini kidogo atamjibu mteja 'kama utaki weacha wenzio watanunua, sisi kila siku ndo tunavyo uza we nenda bwana unatutilia usiku tu, kama huna hela si useme usaidiwe,kukera biashara za wenzako tu'. Ukimkuta mfanya biasha muoga, basi anashindwa hatakumjibu mtejawake, anakasirika kimya kimya, nakesho biashara hiyo anaacha kabisa, kisa "nimekwazwa".
Kama ikikutoke wewe usipandwe na gadhabu jibu ni rahisi tu, kama ni kweli kuna kitu ulikosea mwambie "bwana pamoja na iyo shida kidogo uliyo iyona lakini bidhaa yetu ni bora una jaribu kumwonyesha kwamifano, namna bidhaa yenu ilivyo bora, au pia unamtaka radhi na kumwaidi mara nyingine utajitaidi kuboresha vizuri". Usikasirike ndugu, ingawa ni kweliwateja wengineujui aliko toka, jitaidi kuwa makini.
Kwa leo ni hayo tu ndugu zangu tutaonana wakati na mara nyingine.
Sisi sote ni ndugu,
Godfrey Nangeda
0717008781/0756314274
No comments:
Post a Comment