| Kuna vitu vitatu muhimu sana kwa mtu yeyote anayetaka kufikia mafanikio makubwa. Vitu hivyo ni kufanya kazi kwa bidii na maarifa, kuwa mwaminifu na kuwa muadilifu. Ukikosa kimoja kati ya vitu hivi vitatu ni sawa na jiko la mafiga matatu ambalo limekosa figa moja, haliwezi kupika. Ukikosa vyote vitatu ni sawa na kwamba huna maisha kabisa. Kama ilivyo kwenye jiko kama hakuna mafiga yote matatu hakuna jiko kabisa. Tabia hizi tatu ndio zitakazokuwezesha kutoka popote ulipo, hata pangekuwa chini kiasi gani na kuweze kufikia mafanikio makubwa. Bila ya tabia hizi tatu utajaribu sana kufikia mafanikio lakini utashindwa. Unaweza kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ila kama umekosa uaminifu, hakuna mtu atakayetaka kufanya kazi na wewe. Unaweza kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na ukawa na uaminifu, ila kama umekosa uadilifu utajikuta kila siku unaingia kwenye matatizo. Kutokana na umuhimu wa tabia hizi tatu katika kufikia mafanikio, tutazijadili moja baada ya nyingine hapa kwenye kipengele cha TABIA ZA MAFANIKIO kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Mwezi huu wa pili tutaanza kujijengea tabia ya UAMINIFU. Kwa mwezi mzima kila siku ya jumanne utapata makala itakayokuwezesha wewe kujijengea tabia hii muhimu ambayo itakuwezesha kufikia malengo yako na mafanikio makubwa. Je inawezekana kujijengea tabia hii?Swali muhimu ambalo watu wengi wanaweza kujiuliza ni je inawezekana kujijengea tabia hii? Watu wengi wanafikiri ukishakosa uaminifu na hasa unapokuwa mtu mzima ndio basi tena, ni vigumu kubadilika kwa sababu ndivyo maisha yako yalivyozoea.Ukweli ni kwamba kitu chochote ambacho unakifanya sasa umejifunza hapa hapa duniani. Ni tabia chache sana ambazo mtu umezaliwa nazo, ila nyingine nyingi umejifunza kw akuchagua mwenyewe au kuiga wengine wanavyofanya kwenye jamii inayokuzunguka. Haijalishi umekosa uaminifu kwa muda mrefu kiasi gani, unaweza kuanza kujifunza leo na ukaboresha maisha yako. Katika makala hizi za kujijengea tabia ya uaminifu tutakwenda hatua kwa hatua za jinsi ya kujijengea tabia hii. Kama utafuata maelekezo yote vizuri utakuwa kwenye nafasi nzuri sana ya kufikia mafanikio. Kukosa uaminifu ni tatizo la kitaifa.Kwa nchi yetu Tanzania, kukosa uaminifu ni tatizo la kitaifa. Wizi, ufisadi na hata mambo mengine mabaya yanayoendelea kwenye nchi hii yanatokana na kukosekana kwa uaminifu. Sasa hivi kila mtu anayepata nafasi yoyote anaangalia ni jinsi gani anaweza kupata zaidi ya alichopangiwa kupata. Ndio maana rushwa imekithiri, watu wanaiba fedha na mali za umma na tunaendelea kuwa masikini.Kama tusipoweza kutatua tatizo hili la uaminifu, tutaendele akuwa masikini kama taifa. Hii ni kwa sababu asiye mwaminifu anaendelea kuwa masikini na anawasababisha wengine nao kuwa masikini. Ni muhimu sana kila mtu kujijengea uaminifu.Kwa nchi yetu Tanzania, kila mtu, namaanisha kila mtu anatakiw akujifunza jinsi ya kujijengea tabia ya uaminifu. Sisemi kwamba nchi nzima woote sio waaminifu, ila tuna watu wengi sana ambao sio waaminifu hivyo ni rahisi kuwaharibu wale ambao ni waaminifu. Kwa mfano kwenye eneo ambalo watu wamezoea kutoa rushwa, ukienda mtu ambaye hutoi rushwa unaonekana ni wa ajabu. Hii inaweza kumfanya mtu mwaminifu kutoa rushwa kwa sababu kila mtu anafanya hivyo.Ni muhimu kila mtu kujifunza jinsi ya kujijengea tabia ya uaminifu, ili kama sio mwaminifu uwe mwaminifu na kama tayari ni muaminifu uimarishe uaminifu wako na kuwashawishi wanaokuzunguka nao wawe waaminifu. Watu waliofanikiwa sio waaminifu, sio kweli.Kitu cha mwisho ambacho nafikiri wengi watakuwa wanajiuliza kuhusu tabia hii ya uaminifu ni kwamba mbona watu waliofanikiwa sio waaminifu? Kuna habari nyingi ambazo huwa tunazipata kuhusu watu matajiri, utasikia huyu alifanya mambo fulani ambayo sio ya uaminifu ndio akapata utajiri. Utasikia mwingine amenyonya wafanyakazi, anaibia serikali, anakwepa kodi ndio maana amekuwa tajiri.Kwanzia leo, kama kweli unataka kufikia mafanikio, futa mawazo haya hasi kwenye kichwa chako. Hakuna mtu aliyefanikiwa na akaendelea kukaa kwenye mafanikio hayo kwa muda mrefu kama sio mwaminifu. Mifano iko wazi, angalia viongozi wote wa kiserikali ambao wameiba mafedha mengi na wengine kwenda kuyaficha nje ya nchi kabisa. Mwisho wa siku mambo yamelipuka na ukweli umejulikana. Angalia majambazi ambao wamekuwa wakiiba fedha nyingi bila hata ya kukamatwa, unawez akujiuliza kwa nini watu hawa wasiache wizi baada ya kupata fedha nyingi na kufanya mambo mengine? Jibu ni rahisi, hawan atabia ya uaminifu, hivyo hata akiacha wizi baada ya kupata fedha nyingi na kuingia kwenye biashara anaishia kupata hasara. Leo nakupa siri moja kwa nini watu wengi wenye mafanikio wanajengewa picha kwamba ni watu ambao sio waaminifu. Mwandishi mmoja wa kimarekani aliwahi kuulizwa swali hilo, kwa nini nyie waandishi mmekuwa mkiwaandika watu wenye mafanikio kama watu ambao sio waaminifu. Kwa nini hata kwenye maigizo, watu matajiri wanaonekana kuwa na roho mbaya? Yeye alijibu; hivyo ndivyo jamii inavyopenda kuona, na sisi tunawapatia hicho hicho, pia watu matajiri ni rahisi kuwaandika vyovyote unavyotaka na usipate pingamizi. Ukianza kuwaandika watu masikini, wataleta malalamiko makubwa sana. Ila kwa kuwa matajiri hawana muda wa kufuatilia mambo madogo kama haya basi inakuwa rahisi kwetu. Katika makala hizi za kujijengea tabia ya uaminifu tutajifunz amambo yafuatayo; 1. Maana ya uaminifu. 2. Jinsi ya kujijengea tabia ya uaminifu. 3. Jinsi ya kuepuka mazingira yanayokuondolea tabia ya uaminifu. 4. Uhusiano kati ya tabia ya uaminifu na mafanikio. Kupata nafasi ya kujifunza jinsi ya kujijengea tabia hii ya uaminifu jiunge naKISIMA CHA MAARIFA. Kujiunga bonyeza haya maandishi ya neno KISIMA CHA MAARIFA kisha fuata maelekezo. Jaza fomu na kisha utume fedha ya uanachama kwenda namba 0717396253 au 0755953887 na utume jina au email uliyojiunga nayo. Kupata nafasi ya kujifunza kuhusu tabia za mafanikio na kujifunza ujasiriamali na biashara ada ni tsh elfu kumi kwa mwaka. Jiunge leo ili uweze kupata mafunzo bora yatakayokuwezesha kufikia mafanikio makubwa. Nakutakia kila la kheri kwenye kufikia mafanikio makubwa. TUPO PAMOJA. Makirita Amani, makirita@kisimacha maarifa.co.tz |
Saturday, May 16, 2015
Sunday, May 3, 2015
Who influenced Nyerere: His Ujamaa Philosophy and Azimio Principles?
Waungwana,
Ni nani na ni misingi gani ya utashi iliyojijenga kwenye akili za Julius Kambarage wa Nyerere kutuletea Ujamaa na Kujitegemea na hata Azimio la Arusha?
Wengi tunadhania kuwa ni safari yake ya China 1966. Wengine wanadai ni wale ma-Labor na Socialist wa Uingereza.
Tunajua kuwa tumeangalia sana Ujamaa wetu na Azimio kwa mkao wa Great Leap Forward na Cultural Revolution za China ya Mao na Leninism/Stalinism ya Command Economy, New Economic Policy, Collective farming, na hata matunda ya Bolshevik revolution na sera kama Prodrazvyorstka!
Tukija huku kwetu Afrika tunadai kuna Ujamaa wa Kiafrika, Pan Africanism na mengine mengi.
Lakini bado nafikiri ni kitendawili kwetu kuwa ni ushawishi gani na kwa maono gani Nyerere alikaa chini na kutuletea Ujamaa na Kujitegemea na Azimio la Arusha?
Nikirudia Historia na kuangalia kinachotokea Marekani kiuchumi mwaka huu na nyakati hizi, narudi kujiuliza, falsafa za kiuchumi na kujenga jamii za Marekani zilimkosha Mwalimu Nyerere hasa kuangalia Historia ya great depression?
Je FDR (Franklin Delano Roosevelt) na New Deal yake, Fransiscans/Jesuit philosophy na hata Keynesian Policies zilimbadilisha vipi huyu Mkulu wetu? Planned Economy za National Recovery Administration wakati wa Great Depression ya Marekani na hata Public Works ya Nazi German vilikuwa na nafasi gani?Je alichungulia Front Populaire ya Leon Blum wa Ufaransa na kudonoa mambo kadhaa?
Je kujinasua kwa Marekani baada ya Uhuru wake kutoka Uingereza na kujijenga kama taifa linalojitegemea na si kutegemea falme ya Uingereza na kiburi cha Kimarekani pia kilichangia kumjenga Nyerere kuwa na kiburi cha masikini jeuri?
Twajua Julius Nyerere alikuwa mwana historia mzuri hata ukiangalia na kumpima kutafsiri kwake kwa Julius Kaisari na Mfanyabiashara wa Venisi kazi za William Shakespear zinaonyesha ni influence gani ya fasihi, historia na falsafa alikuwa nayo.
Je Keynes alikuwa na infuence gani kwa Nyerere ambaye alisoma fasihi, historia , uchumi na falsafa alipokuwa Makerere na hata Edinburgh?
What about Wealth of nations, je Nyerere alifanya modification ya principles za Adam Smith akipewa baraka na Labor Party ya Uingereza chini ya ushawishi wa Mama Joy Wickens? Maana ukiangalia Azimio la Arusha, pamoja na kuuzwa kuwa linapiga vita Ubepari, in fact linaruhusu ubepari na mfumo wa Kibepari kwa kiasi fulani hasa linaposema kuwa Viongozi wasiwe na zaidi ya hisa katika makampuni mawili!
Je Plato, Aristotle, Socrates, Ghandi na hata Yesu au Mtume Mohamed wali-play part gani kum-influence Nyerere?
Je alisoma sana Das Kapital na Communist Manifesto ya Karl Marx, akamchanganya Trosky na Friederich Engels?
Je sisi kama Taifa kwa kumfuata Kiongozi wetu tulikuwa ni majaribio (experiment) ambayo mataifa makubwa yalikaa kando kuangalia huyu mwanafalsafa na mwanamapinduzi wa Afrika akikoroga na kuunganisha mifumo ya kiuchumi ya Ubepari, Ukabaila, Ukomunisti na Ujamaa na kuunda Ujamaa wa Kiafrika ambao ulilenga kwenye kujitegema na hata kuzaa Azimio la Arusha kubana tabaka la viongozi na kuhamasisha umiliki wa mali kwa umma na si watu binafsi?
Tumeegemea sana kusema tumeunda Ujamaa wetu kutokana na ziara yake ya China na kuharibika kwa uhusiano wetu na Uingereza kulikotokea kipindi hicho hicho.
Je inawezekana kuwa kiwango kikubwa cha falsafa zake za Ujamaa na Azimio ni mgawanyiko sawa wa influence za magharibi wakati wa depression na mashariki wakati wa uprising na mapinduzi?
Subscribe to:
Comments (Atom)